Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: TPDC YAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI LINDI, YAKABIDHI SHILINGI MILIONI 40 ZA UJENZI WA VYOO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa TPDC Dkt. James Mataragio akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa ...
TPDC
Mkurugenzi wa TPDC Dkt. James Mataragio akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania katika Mkutano wa Diaspora jijini Dar es Salaam. 
(Picha kutoka Maktaba)

Na.Ahmad Mmow, Lindi.
KATIKA kuonesha kuwa inatambua kuwa ubora wa elimu unachingiwa na miundombinu bora katika maeneo ya kufundishia. Shirika la maendeleo ya petroli nchini (TPDC), limekabidhi shilingi 40.00 milioni kwa mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, ili zitumike kwa ujenzi wa vyoo katika shule za msingi nne zilizopo katika wilaya ya Lindi.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa TPDC kwenye hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika jana ofisini mwa mkuu wa mkoa huyo, msimamizi usambazaji wa gesi wa shirika hilo, Ismail Naleja, alisema licha ya kuwa shirika hilo ni mali ya umma lakini pia ni miongoni mwa wawekezaji.

Hivyo linatambua umuhimu wakusaidia upatikanaji wa huduma za jamii katika maeneo wanayofanyia uwekezaji. 

Naleja alisema msaada huo umetolewa baada ya kusikia kuwa shule nyingi katika mkoa huu zinatatizo la uhaba wa vyoo.
"Tunaunga mkono jitihada zako, na sisi kama miongoni mwa wawekezaji hatutaishia hapa kutoa msaada katika kuboresha huduma za jamii, bali tutaendelea," alihaidi Naleja.

Aidha ofisa mwandamizi huyo alitoa wito kwa wanufaika wa misaada mbalimbali, ikiwamo shule za Ingawali, Madangwa, Ng'apa na Mkupama, ambazo zitanufaika na msaada huo watumie kwa kazi zinazokusudiwa.

Ofisa elimu wa mkoa wa Lindi, Gift Kyando alisema upungufu wa vyoo shuleni ni miongoni mwa matatizo yaliyo kwenye sekta ya elimu katika mkoa huu.

Ambapo hadi sasa kuna upungufu wa vyoo 4132 kati ya 7698 vinavyohitajika.
"Mahitaji halisi ni matundu 7698, hata hivyo yaliyopo ni 3566. Upungufu uliopo ni sawa na 53.7% ya mahitaji. Shule ambazo hazina vyoo kabisa ni 51," alisema Kyando.

Nae mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Lindi, Jomary Satura ambae halmashauri yake inashule mbili( za Mkupuma na Ng'apa) zitazonufaika na msaada huo. Alisema kitendo kilichofanywa na shirika hilo licha ya kupunguza uhaba wa vyoo, lakini pia inaonesha ni kwakiwango gani linathamini jamii na kuziona changamoto kujali zilipo katika jamii na hivyo kuchua hatua za kusaidia kutatua.

Hali inayotoa ushahidi kuwa uwekezaji unaofanywa na shirika hilo utaendelea kuwa natija kwa wananchi. 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa, Godfrey Zambi, akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo, alitoa wito kwa shirika hilo kuona namna ya kuwasaidia wananchi waliotoa maeneo yao ili kupisha ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi, wajenge nyumba badala ya kupewa fedha na viwanja kama fidia.

Alisema badala yakuweka kipaumbe katika kuwapa viwanja na fedha lifikirie kuwajengea badala ya kuwapa fedha ili wakajenge wenyewe.

Mbali na wito huo, Zambi alisema bomba la gesi limebeba uchumi wa nchi. Hivyo wahamasishe jamii itambue umuhimu huo ili iweze kushiriki kikamilifu kutunza na kulinda.
*********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top