Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU ANUSURIKA KUFA MARA BAADA YA KUBWAKWA NA KUTELEKEZWA KORONGONI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo Na Woinde Shizza, Meru MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu ...
Charles Mkumbo
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo

Na Woinde Shizza, Meru
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo Meru mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kutelekezwa kwenye korongo la mchanga na kusababishiwa maumivu makali
yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

Akielezea tukio hilo mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa 12.30 alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho
kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimenipelekea nishindwe kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo imeonekana aliniumiza sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu" alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli Akyoo alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani tangu akamatwe mtuhumiwa huyo na kupelekwa kituoni bado hajasomewa shitaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona wako sawa
kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo.

Nae mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus alisema kuwa tukio hilo limemfanya mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo ameshindwa kuendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia nyingine ili kimbadilisha mawazo ya kifikra.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli Matayo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa
jina la Wilson Elias ambae ndie aliyehusika na ukatili huo na kumfikisha katika kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa polisi Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambapo limesema
kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa RB namba RB/R/4250/2016 na atafikishwa mahamani upelelezi ukikamilika.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top