Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WANANCHI WA TARAFA YA RONDO WAIOMBA SERIKALI KUTATUA KERO YA MAJI (+Video)
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
NA FATUMA -LINDI Wananchi wa Tafara ya Rondo, katika Halmashauri ya wilaya ya Lindi, wameiomba ser...
NA FATUMA -LINDI
Wananchi wa Tafara ya Rondo, katika Halmashauri ya wilaya ya Lindi, wameiomba serikali kuwatatulia tatizo la maji ambalo wamekuwa wakitaabika kwa muda mrefu.

Wananchi Rondo
Wakizungumza na Lindiyetu.com, wananchi hao wamesema wanalazimika kumka saa kumi za usiku kutembea kufuata maji umbali wa masaa manne katika kitongoji cha chilala.
Wananchi Rondo
Hata hivyo wananchi hao wamesema wanahatarisha maisha yao kutokana na kuwepo na wanyama wakali kama vile simba, nyoka pamoja na chui huku kina mama wakamuomba makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassani kuwaangalia kinamama wenzake kwa jicho la huruma ambao wamekuwa wakitabika kwa shida ya maji kwa muda mrefu na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo ya kujitafutia kipato cha kila siku hali inayosababisha wananchi kukaa siku nne bila kuoga kutokana na tatizo hilo la maji.


FUATILIA MAHOJIANO YA MOJA KWA MOJA KATIKA VIDEO HAPA CHINI.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top