Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAKULIMA WAPIGA GOTI, WAFUGAJI WADONDOSHA CHOZI MBELE YA MKUU WA MKOA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi Na. Ahmad Mmow, Lindi. KATIKA hali inaoyoonesha kukos...
Godfrey Zambi
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi

Na. Ahmad Mmow, Lindi.
KATIKA hali inaoyoonesha kukosekana mahusiano mema baina ya wakulima na wafugaji wa kata ya Somanga wilaya ya Kilwa. Baadhi ya wakulima na wafugaji wakata hiyo walijitahidi kumshawishi kwa maneno na vitendo mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi awaonee huruma. Huku kila upande ukiutuhumu upande mwingine kuwa ni chanzo kitakacho sababisha uvunjifu wa amani katika kata hiyo.

Hayo yalitokea kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na mkuu huyo wa mkoa, uliofanyika katika kijiji cha Somanga, mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Wakulima waliwatuhumu wafugaji kuwa ni chanzo cha kuvurugika mahusiano mema kutokana na tabia zao za ubabe, ikiwamo kulisha mifugo kwa nguvu kwenye mashamba yao.

Wakati wa wafugaji waliwatuhumu wakulima kuwa wanawatisha wanapo kuwa machungani na kuikatakata kwa mapanga mifugo yao bila sababu.

Baada ya Zambi kutoa nafasi ya kuuliza maswali na kueleza kero zao baada ya kumaliza hotuba yake iliyokuwa imezungumzia maagizo mbalimbali ya serikali na mipango ya maendeleo ya mkoa huo. Ndipo wakulima na wafugaji hao wakaweka wazi kuwa mahusiano baina yao sio mazuri na wanaishi kwa uhasama mkubwa.

Hivyo mkuu huyo wa mkoa aupatie uvumbuzi mgogoro huo. Hata hivyo wakulima na wafugaji hao katika kumshawishi walikuwa wanasema kweli na wanahitaji kuhurumiwa ndipo kila mmoja alitumia mbinu yake kumshawishi.

Aliyeanza kuzungumza kwa upande wawakulima alikuwa, Upendo Ulaya ambae wakati anazungumza alikuwa amepiga magoti na kunyanyua mikono juu mithili ya mkosaji aliyekuwa anaomba radhi mbele ya mtu aliyemkosea.

Pendo alisema wafugaji wamekuwa ni miongoni mwakero zinazohitaji kutatuliwa na mkuu huyo wa mkoa, kwa madai kuwa tatizo hilo lina muda mrefu. Hata hivyo halijapata suluhisho. Alisema wafugaji wanalisha mifugo yao kwenye mashamba wanapowauliza wanajibiwa kuwa mifugo inathamani kuliko mazao ya kilimo na hawaogopi chochote.

Huku akiwa amepiga magoti na kunyanyua mikono juu alisema:
"Baba tuokoe wanao tunapigwa na wafugaji, mazao yetu yanaliwa na ng'ombe. Tukilalamika kwa viongozi wetu tunawekwa ndani, hatuna kwa kwakwenda kulalamika nakusikilizwa hali nimbaya baba," alisema Upendo.

Nae mfugaji Bangili Nganga Mbeho alisema wafugaji hasa vijana wanaochunga mifugo usalama wao upo mashakani.

Kwamadai kwamba wanatishwa na mifugo yao inakatwa na mapanga inapokuwa malishoni. Hata kama haijaingizwa kwenye mashamba. Mfugaji huyo huku akitiririkwa na machozi alisema:
"Wafugaji tunawindwa tunaishi kwa hofu, vijana wetu wakiwa machungani wanatishwa, ng'ombe wetu wanakatwa mapanga. Sisi niwa Tanzania twende wapi mkuu wa mkoa," alilalamika. 

Mfugaji huyo alisema chanzo cha mgogoro ni wakulima kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mifugo nakulima mashamba. Hivyo maeneo yakufugia yamelimwa mashamba, na kusababisha eneo la kufugia kuwa dogo. 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa, Zambi alisema ofisi yake itaunda tume haraka ambayo jukumu lake litakuwa nikubaini chanzo halisi cha mgogoro huo na kushauri njia bora zitakazo tumika kupata suluhisho la kudumu la mgogoro huo. 

Aliwataka wakulima na wafugaji hao kuacha kuhasimiana, waheshimu mipaka iliyowekwa kisheria na waishi kama ndugu. Alisema asingependa kuona wananchi hao wanaishi kwa mfumo huo unaotishia amani na utulivu.

Huku akibainisha kuwa kila mmoja anawajibu wa kuheshimu kazi halali ya mwenzake.
"Kila mmoja ameonesha kuvutia kwake, ni hali inayoonesha kuwa kuna mgogoro, nitaunda kamati ambayo itawashirikisha wawakilishi wa wakulima na wafugaji," alisema Zambi.

Mkuu huyo alitoa ushauri kwa wakulima nawafugaji hao wajenge utamaduni kabla ya kuingia kwenye migogoro, wakulima kilimo cha kisasa iliwaweze kuzalisha mazao mengi kwenye maeneo madogo na wafugaji wafuge kiasi cha mifugo kinachoweza kuhimili maeneo yaliyotengwa kwa ufugaji.

Mgogoro huo uliwahi kuingiliwa kati hivi karibuni na mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai kuagiza wafugaji waache tabia ya kwenda kufugia na kulisha kwenye vijiji na maeneo yasiyotengwa kwa ufugaji na waondoke kwenye maeneo na vijiji hivyo.

Pia wakulima waliovamia na kuweka mashamba kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ufugaji waondoke kwenye maeneo hayo. Agizo ambalo pia limelalamikiwa na baadhi ya wakulima kwenye mkutano huo.
**********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top