Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: WAKULIMA WAGOMA KUUZA KOROSHO MNADANI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Liwale. MNADA wa sita wa korosho  uliotarajiwa kufanyika leo mjini Liwale, umeshi...
Na. Ahmad Mmow, Liwale.
MNADA wa sita wa korosho
 uliotarajiwa kufanyika leo mjini Liwale, umeshindwa kufanyika baada ya wakulima kugoma kuuza.
Korosho
Wakulima hao wakiongozwa na makamo mwenyeti wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Hassan Mpako, walikataa kuuza korosho hizo zilizopo kwenye maghala ya Lindi farmers na Umoja, kutokana na kutoridhishwa na mchakato wa matangazo kwa wafanyabiashara uliosababisha kujitokeza wanunuzi wachache.

Makamo mwenyekiti huyo wa RUNALI, ambae pia ni mwenyekiti wa chama cha msingi cha ushirika cha UMOJA, ndie aliyeanza kuonesha wasiwasi kuhusu jinsi matangazo ya mnada huo yalivyotolewa na kusababisha wajitokeze wanunuzi sita kuomba kununua zao hilo linalozalishwa kwa wingi katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Mpako alisema matangazo ya mnada huo hasa kuhusu kiasi cha korosho zilizotarajia kuuzwa hayakutolewa kwa wakati.

Hivyo kusababisha wanunuzi wengi kukosa taarifa na kusababisha  kujitokeza wafanyabiashara hao wachache ambao hata bei walizoomba kununulia zilikuwa za chini kuliko za minada mitano iliyopita.
"Watendaji wa RUNALI walifanyajitihada kubwa na walitimiza wajibu wao, walishapeleka taarifa mapema bodi ya korosho. Katalogi(orodha ya kiasi cha bidhaa ), hata hivyo katalogi ya bodi  ilipokelewa saa tano na mtandao ulikuwa unamaandishi yasioleweka," alisema Mpako.

Alisema iwapo matangazo yangetolewa mapema kungekuwa na uwezekano wa wanunuzi wengi kujitokeza. Hivyo kungekuwa na ushindani ambao ungesababisha kupandisha bei. 

Akiongeza kusema "Nijambo la kushangaza kusikia kampuni zilizojitokeza kwenye mnada huu ni sita wakati msimu huu kunakampuni 66 ziliomba kununua," alisema.

Mhasibu  wa chama cha msingi Mirindimo, Ahmad Makokola, alisema mfumo wa ununuzi ulipoanza  ulionesha ungekuwa na manufaa kwa wakulima. Hata hivyo kadiri siku zinavyokwenda, matumaini ya kunufaika yanapungua." Kwakuzingatia maelezo ya makamo mwenyekiti, mimi sipotayari kuuza korosho za chama changu kwenye mnada huu, nawashauri nawenzangu tusikubali kuuza.

Nae mwenyekiti wa chama cha msingi cha Mchangani, Maliki Maluchila alisema kutokana na kutoridhishwa na mchakato wa matangazo ya kuwapata wafanyabiashara na bei ndogo, yeye kama kiongozi wa wachama cha msingi ambacho ni mali ya wakulima, hakuwatayari kuuza korosho za wakulima hao katika mnada huo.

Mkulima Abeid Mtamajagi wa kijiji cha Liwale B, alisema hali hiyo inazidi kuwakatishatamaa wakulima na kuwaongezea maumivu. Kwamadai kwamba hata ambao korosho zao zilinunuliwa kwenye minada iliyopita hawajalipwa. 

Alisema hali hiyo itawafanya wauze korosho kwa walanguzi. Kutokana na maelezo ya wakulima hao, mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliunga mkono uamuzi wa wakukulima hao, kwa kukubali mnada huo usitishwe.

Alisema aliamua kwenda kwenye mnada huo kujifunza na kuona jinsi minada inavyo endeshwa. Huku akibainisha kuwa ofisi yake itafuatilia ili kubaini ukweli wa sababu zilizoelezwa. Iwapo nikweli kutokana njama za makusudi zinazofanywa na watu wasio waadilifu ambao  wanataka kujinufaisha kupitia nguvu za wakulima au ni hali ya kawaida ya kibiashara.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amezionya kampuni zinazochelewa kulipa fedha za wakulima kwa wakati ziache tabia hiyo. Huku akiweka wazi kuwa kampuni ambazo hazitakuwa na rekodi mzuri katika kulipa fedha za wakulima kwa mujibu wa makubaliano hazitaruhusiwa kufanyabiashara hiyo katika mkoa huu.

Awali meneja wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Christopher Mwaya, alisema wanunuzi waliojitokeza kwenye mnada huo ni sita. Ambapo bei katika mnada huo zilikuwa ni shilingi 2,953/= hadi 3,276/= kwa kila kilomoja.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top