Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: STAA HUYU WA CLUB YA CHELSEA ATAJWA KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED JANUARY
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Ni mwezi mmoja tu umebaki hadi kufikia mwezi January ambapo dirisha dogo la usajili barani Ulaya ...
Jose Mourinho
Ni mwezi mmoja tu umebaki hadi kufikia mwezi January ambapo dirisha dogo la usajili barani Ulaya litafunguliwa rasmi, bado dirisha la usajili halijafunguliwa lakini headlines za mchezaji gani atajiunga na timu gani mwezi January zina zidi kuchukua nafasi.

Kocha wa Man United Jose Mourinho ameanza kuhusishwa kuwa katika mpango wa kumsajili Willian wa Chelsea mwezi January, stori kutoka dailystar na 101greatgoals.com imeeleza kuwa Mourinho anataka kumsajili Willian ambaye imeanza kuaminika kuwa anakosa nafasi chini ya Antonio Conte.
Willian akiwa na kocha Jose Mourinho wakati wakiwa pamoja Chelsea

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Willian alijiunga na Chelsea August 2013 akitokea klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi aliyodumu nayo kwa kipindi kifupi tu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top