Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: PENGO LA MAREHEMU KANUMBA LITAZIBIKA TU - GABO ZIGAMBA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amef...
Msanii wa filamu anayefanya vizuri na filamu ‘Safari ya Gwalu’ Salim Ahmed aka Gabo Zigamba amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wa filamu wakiwa na juhudi wanaweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba.

Gabo Zigamba

Mwigizaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wa filamu ambao wanafanya vizuri kwa sasa, amedai kama wasanii wakiamua kufanya kazi kwa bidii basi kila kitu kinawezekana.
“Pengo la marehemu Kanumba litazibika tu ingawa najua tobo la panya huwezi kuziba na mkate ila tutajitahidi kuziba,” Gabo alimjibu shabiki katika Kikaango cha EATV.

Aliongea, "Niwashauri watu wawe makini kwenye nidhamu, wawe makini kwenye elimu na pia wasikate tamaa katika mambo wanayofanya"

Mwigizaji huyo amemtaja Single Mtambalike kuwa ndiye mwigizaji wake bora kwa sasa.

***********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top