Fungwa Kilozo Fungwa Kilozo Author
Title: OMMY DIMPOZ AJIBU MAPIGO, AFUNGUKA MAKUBWA KUHUSU UNUNUAJI WA VIEWERS, UCHAWI NA USALITI
Author: Fungwa Kilozo
Rating 5 of 5 Des:
Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM , Ommy Di...
Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.
Ommy Dimpoz
Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi kuzifanya ili kuomba wayamalize.

Hitmaker huyo wa "Wanjera" amesema katika urafiki wao wote na Diamond, ni yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa vinavyohusiana na kazi.

Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake "Tupogo" na kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King Malou. 


Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake ‘Number 1’ katika studio za MJ Records.

SIKILIZA HAPA INTERVIEW YOTE

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top