Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MWANA FA AINGILIA BIFU LA DIAMOND, ALIKIBA NA OMMY DIMPOZI- AYANENA HAYA (VIDEO)
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mwana FA ameonya kuhusu bifu zinazoendelea kwenye muziki wa Bongo Flava kwamba zinakoelekea, watu...
Mwana FA ameonya kuhusu bifu zinazoendelea kwenye muziki wa Bongo Flava kwamba zinakoelekea, watu wanaweza kufanyiana vitu vya hatari zaidi.
Mwana FA
Akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV leo, FA amesema busara zinahitajika kumaliza tofauti baina ya wasanii wanaohusika kwenye bifu hizo.

“Tufike mahali kwamba tujiwekee mipaka kama binadamu kwamba hivi vitu ambavyo tunaambiana kama ungekuwa unaambiwa wewe na familia yako ingekuwa sawa? Maana yake tunavyoelekea tutatoana macho hivi karibuni,” alisema rapper huyo.

“Watu pekee wanaoweza kufanya ni wao wenyewe wanaohusika. Nafikiri watu wawe humble, warudi chini kidogo, wanaelea sana juu, turudi chini kidogo, tujikumbuke sisi nani na kama malengo yetu ni kutoana roho ama kuendelea kufanya muziki tuweze kujitengenezea vipato,” amesisitiza.

Ushauri wa Mwana FA umekuja katika wakati ambao uhasama kati ya kambi ya Diamond na Alikiba unazidi kushika kasi.

Rapper huyo ameachia video ya wimbo wake mpya "Dume Suruali" aliyomshirikisha Vanessa Mdee.
********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top