Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MANJI AKUTANA NA RUNGU KALI LA SERIKALI YA JPM
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Ardhi, jijini Dar es Salaam, imeamuru Kampuni ya Quality Group inayom...
Yusuph Manji
MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Ardhi, jijini Dar es Salaam, imeamuru Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na mfanyabishara Yusuph Manji na wenzake kuondoka kwenye jengo la Quality Plaza na kulipa kodi ya pango wanayodaiwa tangu mwaka 2007 mpaka sasa.

Fedha hizo zitalipwa kwa mlalamikiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo, Kampuni ya Image Properties and Estate ambayo ni wakala wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), unaomiliki jengo hilo.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Msajili wa Mahakama hiyo, Frank Mahimbali, kwa niaba ya Jaji John Mgetta katika kesi nne zilizofunguliwa na Kampuni ya Quality Group kupinga kulipa kodi ya jengo hilo.

Kesi hizo zilitokana na mdai Quality Group kukimbilia Mahakamani kufungua shauri jipya kila alipokuwa akipelekewa notisi ya kuhama katika jengo hilo na mlalamikiwa wake, Kampuni ya Image Properties and Estate.

Source: Nipashe

********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top