Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: JOKATE AZIDI KUMWAGIA SIFA MPENZI WAKE ALIKIBA, AYASEMA HAYA TENA.
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamitindo maarufu Jokate Mwegelo  amefunguka ya moyoni na kumwaga sifa za kutosha kwa mwanamuzi...
Mwanamitindo maarufu Jokate Mwegelo amefunguka ya moyoni na kumwaga sifa za kutosha kwa mwanamuziki Alikiba kutokana na uwezo wake kisanaa na namna anavyoendesha maisha yake.
Jokate Mwegelo na Alikiba
Jokate amesema kuwa kimuziki anaweza kumfananisha Alikiba na msanii Beyonce kwani ana uwezo mzuri wa kuimba live kwa sauti nzuri, kucheza, kurap na kucheza na mashabiki pindi awapo stejini.

Jokate alimwaga sifa hizo kupitia mtandao wake wa Instagram na kuwataka mashabiki wa Alikiba kumlazimisha msanii huyo aweze kufanya "tour" yake mwenyewe nchi nzima ili aweze kuwafikia mashabiki wengi zaidi ambao wana kiu ya kupata burudani kutoka kwake.

Ujumbe ulisomeka hivi

“Naomba kusema tu wewe hushindani na yoyote hapa Tanzania, kuanzia ladha yako ya muziki unaotengeneza mpaka sauti yako, tena huko kwenye sauti naomba nisiongee maana sitaki upasuke bichwa lako lol ila kuna kitu cha kipekee kwenye sauti yako, you are “The Voice”. Kila siku unakuwa bora zaidi yaani labda nikufananishe na Beyonce kimuziki, usiniue lakini. Ukitaka you can dance, you can sing tena live sauti clear haina mikwaruzo, you can rap, unaweza igiza uchizi yaani you are just perfect kama mwanamuziki. Kama hujui leo ujue. Nakuombea siku moja dunia nzima iweze kufurahia hiki kipaji adhimu kutoka kwako” aliandika Jokate
************** 

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top