Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: ILE SKENDO YA VANESSA MDEE KUTOKA NA TREY SONGZ YALETA FAIDA KWA VEE MONEY
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki wa Bongo fleva, mwana dada Vanesa Mdee a.k.a Vee Money , amefunguka na kueleza f...
Msanii wa muziki wa Bongo fleva, mwana dada Vanesa Mdee a.k.a Vee Money, amefunguka na kueleza faida alizopata kwa kuwa karibu na nyota wa muziki nchini Marekani Trey Songz.
Vee Money
Akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, Vanessa alitakiwa kueleza faida alizopata kutokana na skendo zilizovuma siku za hivi karibuni kuwa alitoka kimapenzi na Trey Songz kipindi walipo kuwa nchini Kenya katika Coke Studio.

Katika majibu yake, Vanessa alisema kuwa hakuna jambo linalovuma kwake bila ya kuwa na faida, na kwamba skendo hizo zilivuma hadi Marekani, kwani aliandikwa katika baadhi ya blogs za Marekani kuhusu ukaribu wake na Trey Songz, kitu kilicho mfanya kujulikana hadi katika taifa hilo lenye nguvu katika karibu kila nyanja, ikiwemo muziki duniani.

Trey Songz na Vanessa Mdee
Miezi kadhaa iliyopita ziliibuka tetesi, picha na video zilizosambaa mitandaoni zinazoonesha ukaribu kati ya nyota wa muziki wa R&B nchini Marekani, Trey Songz na Vanessa Mdee, zilizotafsiriwa kuwa huenda wakawa wameenda hatua ya juu zaidi ya kile walichokuwa wakikifanya Nairobi, Kenya.

Tetesi hizo zilikuja kipindi Vanessa pamoja na wasanii wengine takriban 9 wa Afrika, waliingia studio na Trey Songz kurekodi wimbo kwaajili ya msimu mpya wa kipindi cha Coke Studio Afrika. Hata hivyo Trey alionekana kuwa karibu zaidi na Vee Money kiasi cha kuzusha tetesi kuwa huenda Jux akawa amesalitiwa.

Trey Songz na Vanessa Mdee
Vee alisema picha na video hizo zilitafsiriwa vibaya na kwamba yeye na Trey wamewahi kukutana kabla ya hapo na siku zote amekuwa karibu naye.

Trey Songz amekuwa akifananishwa kimuonekano na mpenzi wa Vanessa, Jux licha ya Jux mwenyewe kuweka wazi kuwa Trey Songz ndiye role model wake.

*******

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top