Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HATA MBELE KUNA KUZIMIWA MIC SIO KENYA TU, AUGUST ALSINA YEMEMKUTA KWENYE USIKU WA TUZO ZA AMA's
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Usiku wa tuzo za America Music Awards, August Alsina alipangiwa kufanya perfomance pamoja na Dj Kh...
August Alsina
Usiku wa tuzo za America Music Awards, August Alsina alipangiwa kufanya perfomance pamoja na Dj Khalid rapper Future na wengine, lakini kilichomshangaza ni baada ya Mic yake kuzimwa na kumfanya yeye agande tu stejini bila kuimba, kitu ambacho anasema kimemfanya ajisikie vibaya sana ukizingatia kila kitu kilikuwa live kwenye Tv.
August aliandika kwenye Instagram yake na kusema japokuwa anashukuru kwa nafasi hiyo aliyopata lakini hakufurahishwa na kitendo cha yeye kuzimiwa mic akiwa jukwaani kwani amekuwa akifanya mazoezi wiki nzima kwaajili ya usiku huo.
Hata hivyo August alishukuru uwepo wa Dj Khalid ambaye alimtambulisha kama kaka yake na kusema kwakuwa wimbo wao wa ‘Do You Mind’ unashika namba moja Marekani anashukuru pia.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top