Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: FIESTA 2016 IMOOOOOOO.....!! YAMTAMANISHA RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema alitamani kuhudhuria tamas...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema alitamani kuhudhuria tamasha la muziki la Fiesta ambalo litafanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club.
Dkt John Pombe Magufuli
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii Ikulu jijini Dar es salaam, Magufuli alisema alitamani kuhudhuria tamasha hilo ili apige tumba lakini majukumu ya kazi yamembana.

“Natamani kwenda Fiesta siku ya kesho sema hii kazi inanibana kwa kuwa itakuwa live nitaifuatilia kupitia kwenye runinga,” alisema Magufuli.

Pia Rais huyo ambaye kesho November 5 anatimiza mwaka mmoja toka aingie madakani, alimmwagia sifa msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kwa kufanya muziki wenye maadili na kuelimisha.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top