Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: CHADEMA WAMFUKUZA UANACHAMA ALIYEGOMBEA UBUNGE SONGEA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Songea Mjini, kimemvua uanachama aliyekuwa...
Chadema
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Songea Mjini, kimemvua uanachama aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Songea Mjini, Joseph Fuime, kwa tuhuma za makosa mbalimbali, likiwamo la kukihujumu chama hicho.
Katibu wa Chadema Wilaya Songea Mjini, Olais Ng’ohison, alisema Fuime amefutwa kwenye orodha ya wanachama wa chama hicho tangu Oktoba 23, mwaka huu.

Alisema chama kimelazimika kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kuwajuza wananchi, wadau, wakereketwa na viongozi mbalimbali baada ya kubaini kuwa watu wengi walikuwa hawafahamu kuwa Fuime ameshafutwa uanachama.
Kwa mujibu wa katibu huyo, Fuime katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka jana alikuwa mgombea ubunge lakini alikihujumu chama kwa mambo mbalimbali yakiwamo ya kutoshiriki katika majumuisho ya kura kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea na aliamua kuzima simu zake bila sababu za msingi.

**********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top