Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: ALIKIBA AMEANDIKA UJUMBE HUU BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI HALALI WA TUZO YA MTV EMA BEST AFRICAN ACT 2016
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Imetangazwa rasmi na waandaaji wa tuzo hizo za MTV EMA kuwa Msanii Alikiba ndiye mshindi halali ...
Imetangazwa rasmi na waandaaji wa tuzo hizo za MTV EMA kuwa Msanii Alikiba ndiye mshindi halali wa tuzo ya MTV EMA category ya Best African Act.
Alikiba MTV EMA Best African Act
Kupitia kurasa yake ya Instagram Alikiba ameamua kuchukua nafasi ya kuwashukura watu wake wa karibu pamoja na mashabiki zake kwa sapoti ambayo wanampa hadi kuhakikisha ameipata tuzo hiyo.
Alikiba MTV EMA Best African Act
"Namshukuru MUNGU Na Shukrani kwa MTV kwa heshima hii, nina furaha sana kwa ushindi huu, ni heshima kwangu na nchi yangu Tanzania 🇹🇿 pamoja na East Africa nzima kiujumla. Shukrani sana kwa familia yangu, management yangu na mashabiki zangu wote - nawapenda sana" ameandika Alikiba.


Ningependa pia kuchukua nafasi hii kushukuru vyombo vya habari vyote, watangazaji, waandishi na wadau wote wa sanaa kiujumla kwa kunisapoti katika kazi zangu.
Lastly, nawashukuru wasanii wenzangu wote mlionipa ushirikiano na kuthamini kipaji changu kwa kuniombea kura zilizonipa ushindi. Ushindi wangu ni ushindi wa sanaa yetu sote. Proudly Tanzanian 🇹🇿
MUNGU awabariki sana. #TupoPamoja#Kajiandae #KingKiba -
aliongeza Alikiba
**********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top