Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAZIRI MKUU ASIKITISHWA NA BODI YA KOROSHO KUPUUZA MAAGIZO YA SERIKALI.
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea. WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesikitishwa na kitendo cha bodi ya ko...
Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesikitishwa na kitendo cha bodi ya korosho cha kushindwa kufanyia kazi maagizo ya serikali. Badala yake imejipa kazi ya kusimamia minada ya mauzo ya korosho badala ya vyama vikuu.
Kassim Majaliwa
Majaliwa alieleza masikitiko hayo alipokuwa anazungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo mjini Nachingwea. 

Waziri mkuu huyo ambae licha ya kusikitishwa na bodi kwa kitendo hicho, amemuagiza waziri mwenye dhamana ya kilimo na ushirika afanye marekebisho ya watendaji wa bodi hiyo na bodi yenyewe, alisema bodi hiyo ilipewa maagizo ya kwenda kutoa elimu kwa wakulima kuhusu mifumo mbalimbali ikiwamo wakulima kufungua akaunti benki.

Hata hivyo haijafanya hivyo. Badala yake imejipa jukumu la kusimamia minada ya mauzo ya zao hilo badala ya vyama vikuu vya ushirika. Alisema bodi ilitakiwa kuwaelimisha wakulima kuhusu mfumo huo wa malipo badala ya kukurupuka nakuwataka hata wakulima wanaozalisha korosho chache walipwe kwa mfumo huo. Kwa madai kwamba wanatekeleza maagizo ya serikali wakati wanajua serikali haijatoa maagizo ya aina hiyo.
"Wanashindwa kujitetea wanadai wanatekeleza maagizo ya waziri mkuu,niliwaagiza lini na wapi! yakiwashinda wanawasingizia viongozi wa juu,mtu anakilo tano unamlazimisha afungue akaunti sidhani kama nisawa," alisema.

Alibainisha kwamba nia ya serikali kwa wakulima ni njema. Hata hivyo bodi nyingi, ikiwamo bodi hiyo zimekuwa na tabia ya kuharibu na kusababisha malalamiko na matatizo mara kwa mara baina ya wakulima dhidi ya serikali. Hivyo serikali haiwezi kuendelea kuvumilia hali hiyo.

Majaliwa akionesha dhahiri kuchukizwa na mwenendo wa bodi hiyo aliongeza kusema bodi ni vyombo vya serikali ambazo vinawajibu wakutekeleza maagizo yake badala ya kupuuza na kufanya mambo yasio agizwa.
"Mlipewa maagizo tangu mwezi Aprili mkatoe elimu, muda ambao ungetosha hadi kufikia leo, hata hivyo hamjetekeleza na hamjaenda vijijini badala yake mnafanyakazi ya kusimamia minada wakati sio jukumu lenu," alisema. 

Kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa bodi mbalimbali, waziri mkuu huyo amesema serikali itazipitia bodi zote ilikuzibaini ambazo zimeshindwa kukidhi mahitaji na lengo la serikali la kuundwa kwake. Huku akihaidi kwamba Serikali itaendelea kuwashugulikia wanaovuruga ushirika, kwakuanza kusafisha kuanzia wizarani hadi chini.
"Tutazipitia bodi zote, zitakazobainika kuwa ni mbovu tutazivunja na tunaanza na bodi ya korosho,"  alisisitiza.

Waziri Majaliwa ameanza ziara yake ya siku nne katika mkoa huu wa Lindi katika wilaya ya Nachingwea. Ambapo kabla ya kuzungumza na wananchi hao, alizungumza na watumishi wa serikali kupitia mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha walimu cha Nachingwea.

BOFYA PLAY KUTAZAMA VIDEO HAPO CHINI.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top