Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WATAKIWA KUZISIMAMIA KWA UKARIBU HALMASHAURI.
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Chiwanga ambaye nim...
Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Chiwanga ambaye nimiongoni wa viongozi wa mkoa wa Lindi waliofika katika kiwanja cha ndege Nachingwea kumpokea Waziri mkuu na mkewe Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ambao wamewasili katika Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Ruwangwa.


Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
WAKUU wa mikoa na wilaya nchini, wametakiwa kusimamia na kufuatilia yanayofanyika katika halmashauri zilizopo kwenye maeneo yao ya utawala.

Agizo hilo limetolewa leo mjini Nachingwea, na waziri mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza na watumishi kwenye ukumbi wa chuo cha walimu Nachingwea.

Waziri mkuu Majaliwa alisema wakuu wa wilaya na mikoa wanawajibu wakufuatilia na kuhoji yanayofanyika kwenye halmashauri ili waweze kujua yanayoendelea. Ikiwamo matumizi ya fedha zinazopelekwa kwenye halmashauri.

Alisema wakuu hao wanahaki yakuhoji na kujua yanayofanyika na hawana mipaka katika kutekeleza wajibu huo kwa sababu ni wasimamizi wa halmashauri zilizopo katika maeneo yao.

Hivyo wakurugenzi wanawajibu wakusikiliza na kutekeleza maagizo yao.
"Wakuu wa wilaya na mikoa mhakikishe miradi inakamilika na gharama zinalingana thamani halisi, " ili kujua hayo nilazima mufuatilie na hakuna mipaka katika kutekeleza wajibu huo," alisema.

Majaliwa aliwataka pia madiwani kuhakikisha fedha zinatumika na kupelekwa kwenye kazi zinazokusudiwa. 

Akibainisha kwamba baadhi ya halmashauri zimekuwa natabia ya kurejesha fedha hazina kutokana na kutotumika. Kwasababu baadhi ya wakurugenzi wasio waadilifu wanazihamisha na kuzipeleka kwenye akaunti maalumu kwa lengo la kupata faida.

Aidha mkuu huyo wa shuguli za serikali bungeni amezitaka halmashauri nchini zijikite katika kukusanya mapato ya ndani, kupitia na kubuni vyanzo vipya iliziweze kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.
"Halmashauri zinawataalamu watumike kubuni vyanzo vipya vya mapato, ili kutekeleza miradi kwa ajili ya wananchi, kamilisheni viporo na muanzishe miradi mipya," alisisitiza Majaliwa.

Katika hatua nyingine, waziri mkuu huyo amempa mwezi mmoja mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, ahakikishe hospitali ya wilaya ya Nachingwea inafungwa mashine ya kiiletroniki kwa ajili ya kukusanyia mapato ili kudhibiti mapato yanayotokana na uchangiaji unaofanywa na wananchi wanaohitaji matibabu.

Alitoa agizo hilo alipotembelea hospitalini hapo na kuzungumza na watumishi wa hospitali hiyo.
*****************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top