Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAHARIBIFU WA MAZINGIRA WAKAMATWE-MAJALIWA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmed Mmow, Ruangwa. Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi mkoani Lindi kutunza na...
Na. Ahmed Mmow, Ruangwa.
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi mkoani Lindi kutunza na kulinda misitu ili kuiepusha nchi kuwa jangwa.
Kassim Majaliwa
Majaliwa ametoa onyo hilo leo kwa nyakati tofauti, alipozungumza na wananchi katika vijiji vya Nanjalu, Nambilanje, Mkalanga, Namichiga, Nandenje na Mandarawe vilivyopo katika wilaya ya Ruangwa.

Waziri Majaliwa ambae pia ni kiongozi wa shuguli za serikali bungeni, alisema uharibifu wa misitu licha ya kuharibu mazingira, lakini pia unasababisha serikali kutumia fedha nyingi katika kufanya tafiti na kuchimba visima vya maji kutokana na vyanzo vingi vya maji kukauka.

Alisema hali ya uharibifu wa misitu ikiendelea, kunauwezekano mkubwa wa nchi kugeuka jangwa. Hivyo kila mwananchi anawajibu wakuilinda na kuitunza.

Alisema ili kukabiliana na hali hiyo kunahaja ya wananchi kuanza kujenga tabia ya kupanda miti. Huku akiwataka waache kuamini na kuzifanyia kazi mila potofu zinazosababisha uharibifu wa misitu.

Ikiwamo wachome moto misitu ili wajue kama watakuwa na uhai mrefu au mfupi kwa kuangalia kasi na umbali wa moto unapoishia.
"Ukataji wa miti unamadhara makubwa,acheni kilimo cha kuhamahama limeni sehemu moja watumieni na wasikilizeni wataalamu wa kilimo," alisema Majaliwa.

Katika kuhakikisha agizo lake linatekelezwa na kufanyiwa kazi, amemtaka mkuu wa mkoa huu, Godfrey Zambi kutowavumilia watu watakaobainika kushiriki kwa njia yoyote kuharibu misitu. Bali awachukulie hatua kali za kisheria.

Katika hatua nyingine, waziri mkuu Majaliwa amezitaka halmashauri na wakala wa barabara(TANROADS) katika mkoa huu, kumaliza matengenezo ya barabara katika maeneo korofi kabla ya msimu wa mvua kuanza.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top