Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAFANYABIASHARA WANAONUNUA KOROSHO KWA MAGENDO KUTAIFISHWA MALIZAO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mibure wilaya ya Ruangwa na ...

Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mibure wilaya ya Ruangwa na Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwataka wanunuzi wa korosho kufuata taratibu za ununuzi wa korosho ili wakulima wafaideke na zao hilo vinginevyo serekali haita sita kutaifisha magari pikipiki zitakazo kamatwa kubeba korosho walizo nunua kwakutumia utaratibu wa Kangomba.
Picha na Chris Mfinanga

Na. Mwandishi Wetu, Lindi.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi kuhakikisha anadhibiti wafanyabiashara wanaonunua korosho kwa njia ya magendo na atakayekamatwa achukuliwe hatua.

Pia amewataka wananchi wa mkoa huo kutouza korosho zao kwa walanguzi maarufu kangomba na badala yake wazipeleke kwenye masoko rasmi ili waweze kupata tija.

“biashara ya kangomba ni mwiko atakayekamatwa amebeba korosho za kangomba atachukuliwa hatua za kisheria na chombo chake cha usafiri kitataifishwa” amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Oktoba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Mibure, Namakuku, Ng’imbwa, Chienjele, Mkata, Mitope na Kitandi

“Marufuku kuuza korosho kwa kangomba kwani mnapata hasara kipimo kinachotumika si rasmi. Mkoa kamateni na taifisheni korosho na chombo cha usafiri kitakachotumika kubeba korosho za magendo,” amesema.

Amesema ni vema wakulima wakaachana na biashara ya kangomba kwa sababu haina tija na badala yake wasubiri na kwenda kuuza korosho zao katika minada kwa bei nzuri.

“Mwaka huu korosho itauzika kwa bei ya juu zaidi isiyopungua sh.3500, msikubali kuuza korosho mlizizitolea jasho kwa walanguzi wanaotumia kangomba kwa sh. 1000 huu ni wizi, kwani kile kipimo cha wanachotumia ni sawa na kilo mbili, hivyo unapoteza zaidi ya sh. 6000”. amesema

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao kuongeza idadi ya mazao ya biashara na kuanza kulima alizeti ambapo wataweza kupata faida ya zaidi ya sh. milioni moja kwenye shamba la ukubwa wa ekari moja.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa miezi miwili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue kuhakikisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mibure unakamilika.

“Ndani ya miezi miwili Zahanati iwe imekamilika, tuache kuzungumza sasa ni vitendo tu” amesema.
*************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top