Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: VIDEO: YCEE AUNGANA NA DJ MAPHORISA WA AFRIKA KUSINI KUTENGENEZA REMIX YA OMO ALHAJI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa Hip-hop wa Nigeria, Ycee ameungana na mtayarishaji wa muziki na muimbaji wa Afrika Kusi...
Msanii wa Hip-hop wa Nigeria, Ycee ameungana na mtayarishaji wa muziki na muimbaji wa Afrika Kusini, DJ Maphorisa kwenye remix ya wimbo wake unaofanya vizuri barani Afrika, ‘Omo Alhaji’.
Omo Alhaji
Ikifanyika jijini Johannesburg, na kuongozwa na La Dupont Productions, remix ya wimbo huo inahusisha rap iliyoshiba na inayohitaji usikivu.

DJ Maphorisa amechanganya ladha ya kipekee ya Kusini kwenye mrindimo unaoungana vyema na mtindo wa Ycee na kuzalisha wimbo utakaofanya vizuri kwenye klabu, mtaani na hata kwenye redio. Remix hii ya Omo Alhaji, haina shaka itateka tena mawimbi ya redio na TV barani Afrika.

Ycee anasema, “Limekuwa jambo kubwa kufanya remix hii, kama msanii ninafurahi kujaribu muziki tofauti. Ulikuwa uzoefu mkubwa na wa kufurahia kufanya kazi na DJ Maphorisa. Ninaamini mashabiki watafurahia remix hii.”

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top