Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: SIMBA SC YAJIHAKIKISHIA KUENDELEA KUONGOZA LIGI, BAADA YA KUPATA DROO DHIDI YA YANGA LEO TAIFA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mechi ya Vigogo na Watani wa Jadi, Yanga na Simba , iliyochezwa Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar e...
Yanga na Simba
Mechi ya Vigogo na Watani wa Jadi, Yanga na Simba, iliyochezwa Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ikibatizwa Dabi ya Dar es Salaam, ikiwa ni Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, ilimalizika kwa Sare ya 1-1 huku Simba wakicheza kwa muda mrefu Mtu 10 na kusawazisha zikibaki Dakika 3 tu.

Yanga ndio waliotangulia kufunga Bao katika Dakika ya 26 kupitia Amisi Tambwe aliekontroli Mpira wa Pasi ndefu ya Mbuyu Twite na kugeuka haraka na kumchambua kama karanga Kipa wa Simba Vincent Angban.
Yanga na Simba
Bao hilo lilizua hasira kwa Wachezaji na Mashabiki wa Simba wakidai Tambwe alicheza Mpira kwa Mkono na rabsha zikamfanya Kepteni wa Simba Jonas Mkude ale Kadi Nyekundu toka kwa Refa Martin Saanya.

Jukwaani, Mashabiki wa Simba wakaheuka na kuleta vurugu na kuvunja Viti na Gemu kusimama kwa Dakika kadhaa Polisi wakiingilia kati.
Yanga na Simba
Hadi Mapumziko Yanga 1 Simba 0.

Kipindi cha Pili, Yanga wakionekana kuridhika na Bao lao, Simba walijipanga upya na hatimaye kusawazisha Dakika ya 87 kwa Kona iliyopigwa na Shiza Kichuya na moja kwa moja kutinga wavuni huku Kipa Ali Mustapha ‘Barthez’ akipungia hewa na kumuiga Barthez mwenzake wa Man United kutoa ‘maboko’ katika Mechi muhimu.
Yanga na Simba
Matokeo haya yanaendelea kuwafanya Simba wakae kileleni wakiwa na Pointi 17 kwa Mechi 7 na Yanga kubaki wa 3 wakiwa na Pointi 11 kwa Mechi 6.

Timu ya Pili ni Stand United wenye Pointi 12 kwa Mechi 6 wakifuata Azam FC na Mtibwa Sugar wote wakiwa na Pointi 10 kila mmoja na wamecheza Mechi 6 kila mmoja.
Yanga na Simba
VIKOSI: YANGA: Ali Mustapha, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Vicent Bossou, Kelvin Yondani [Andrew Vincent], Mbuyu Twite, Juma Mahadhi [Simon Msuva], Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Deus Kaseke [Haruna Niyonzima]
Akiba: Deogratius Munishi, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Simon Msuva, Hartuna Niyonzima, Obrey Chirwa, Yusuf Mhilu

SIMBA SC: Angban, Mwanjale, Lufunga [Juuko], Bakungu, Zimbwe Jumior, Mzamiru, Mkude, Kazimoto, Kichuya, Mavugo [Blagnon], Ajib Mohammed Ibrahim
Akiba: Manyika, Banda, Mohammed, Ndemla, Juuko, Blagnon, Mnyate

REFA: Martin Saanya

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top