Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: SIMBA SC YAIFUMUA BULA HURUMA TOTO AFRIKA YA MWANZA 3-0
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba iliyokuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza um...
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba iliyokuwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli tatu kwa bila.
Mzamiru Yassin
Ushindi wa Simba umepatikana kupitia Mzamiru Yassin akifunga magoli katika dakika ya 42 na 74, na goli lingine likifungwa na mchezaji raia wa Burundi, Laudit Mavugo katika dakika ya 51.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama 29 ikiongoza msimamo wa VPL, imecheza michezo 11 na ikiwa na mchezo mmoja mkononi, nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga yenye alama 21 huku Toto Africans ikisalia mkiani na alama nane katika michezo 12.

Mchezo unaofuatia kwa Simba ni Jumamosi ya Oktoba, 29 dhidi ya Mwadui ya Shinyanga.

MSIMAMO WA LIGI YA VODACOM HIVI SASA
VPL msimamo

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top