Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MANCHESTER UNITED YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI, YAKUBALI SULUHU DHIDI YA STOKE CITY
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Manchester United imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Stoke City katika mechi amb...
Klabu ya Manchester United imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Stoke City katika mechi ambayo Manchester United iliotawala mchezo kwa kipindi cha mda mrefu.
Manchester United
Baada ya kipa wa Stoke kuokoa mashambulio mengi katika kipindi cha kwanza cha mechi, United ilijiweka kifua mbele baada ya mchezaji wa ziada Anthony Martial kufunga bao la kwanza.
Manchester United
Ilikuwa pigo kubwa kwa Stoke ambayo ilikuwa haijafanya shambulio lolote katika ngome ya United.

Lakini baada ya Jon Walters kupiga krosi, Allen alifika na kusawazisha hivyo basi kuifunga midomo ya mashabiki wa United ambao walikuwa wakiimba katika kipindi chote cha mchuano huo.
Manchester United
Stoke City ambayo iko katika nafasi ya pili kutoka mwisho sasa imejiongezea matumaini ya kuondoka katika eneo la mkia la ligi hiyo ya Uingereza.


VIKOSI: MAN UTD (4-2-3-1): De Gea, Valencia, Smalling, Bailly, Blind, Herrera (Depay 83), Pogba, Lingard (Martial 67), Mata 7 (Rooney 67), Rashford, Ibrahimovic.
AKIBA WASIOTUMIKA: Carrick, Romero, Fellaini, Darmian

STOKE CITY (4-2-3-1): Grant, Johnson, Shawcross, Martins Indi, Pieters, Cameron, Whelan, Shaqiri (Bardsley 90), Allen, Arnautovic (Walters 77), Bony (Crouch 77)

AKIBA WASIOTUMIKA: Adam, Diouf, Given, Krkic

REFA WA MCHEZO: Robert Madley

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top