Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: KATIKA KUMUENZI BABA WA TAIFA, RC ZAMBI AHIMIZA UADILIFU NA UZALENDO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi  Na.Ahmad Mmow, Nachingwea. KATIKA kumuenzi baba wa ta...
Godfrey Zambi
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi 

Na.Ahmad Mmow, Nachingwea.
KATIKA kumuenzi baba wa taifa, hayati mwalimu Julius Nyerere. Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewataka wananchi mkoani humu kuepuka vitendo vinavyopingana na maadili ya kazi na uzalendo.

Zambi alisema hayo kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa taifa, yaliyofanyika leo mjini Nachingwea. 

Alisema ingawa mwalimu hakupenda na aliichukia rushwa hata hivyo baadhi ya watumishi wa umma na wananchi wanapenda rushwa nakuwa kikwazo katika kufikia maendeleo na ustawi wa nchi.

Akibainisha kuwa miongoni mwa sababu nchi ya kushindwa kusonga mbele kwakasi kubwa ya maendeleo ni rushwa na ufisadi unaotokana na tamaa ya baadhi ya watu ambao pia hawana uzalendo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema wananchi na watumishi wa umma wangeishi kwa kuzingatia mfumo wa maisha ya mwalimu, nchi hii ingekuwa mbali kimaendeleo.
"Sina uhakika kama wa Tanzania wa leo tunaishi maisha ya mwalimu, wangapi hatupokei wala kutoa rushwa" mtu ambae sio muadilifu hafai kuwa kiongozi wala mtumishi wa umma," alisema Zambi.

Mkuu wa mkoa alitoa wito kwa viongozi na watumishi wa umma watekeleza na kutimiza majukumu yao kwa ufanisi na uadilifu ili wakumbukwe kwa wema badala ya ubaya. 

Aidha  alitumia nafasi hiyo kuwaagiza wakuu wa wilaya za mkoa huu waige kitendo cha mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango cha kuandaa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa katika wilaya zao.

Licha ya maadhimisho hayo kunogeshwa na burudani na michezo mbalimbali, lakini pia  yalikwenda sanjari na uchangiaji damu na upimaji afya kwa hiari. Ambapo wananchi walipata nafasi ya kupimwa msukumo wadamu, kisukari na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top