Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: JULIO 'ATANGAZA' KUJIUZULU BAADA YA KICHAPO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
KOCHA mkuu wa Mwadui FC  Jamhuri Kihwelo (Julio) amesema atajiuzulu kufundisha soka muda wowote ku...
KOCHA mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo (Julio) amesema atajiuzulu kufundisha soka muda wowote kuanzia sasa kwavile amechoshwa na maamuzi mabovu ya marefarii wa hapa nchini.
Jamhuri Kihwelo (Julio)
Akizungumza kwa hasira baada ya kumalizika kwa mchezo ambao timu yake ilipigwa bao 1-0 na Mbeya City kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya, Julio alisema haoni sababu ya kuendelea kufundisha wakati tayari waamuzi wana matokeo yao.

"Natumia nguvu nyingi kufundisha, kampuni inatumia pesa nyingi kugharamia timu, tunasafiri safari ndefu halafu mwisho wa siku waamuzi wanafanya upendeleo wa waxiwazi.

"Nimeshachoka, nawatazama tu sasa na uamuzi wangu ni kuacha kufundisha mpira, na hii yaweza kuwa mechi yangu ya mwisho kuwa kocha," alisema Julio.

Bao pekee katika mchezo huo liliwekwa nyavuni na Ditram Nchimbi 'Ditinho' aliyeachia shuti kali lililomshinda kipa Shaban Kado na kutinga wavuni.

Mbeya City walitawala mchezo kwa kiasi kikubwa na kuwapoteza Mwadui ambao hawakuonyesha kandanda safi kama ilivyotarajiwa na wengi.

***********************
MAGOLI YOTE YA MECHI YA SIMBA NA YANGA OCTOBA 1 TAIFA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top