Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: JOSE MOURINHO AMTUNISHIA MISURI JURGEN KLOPP NA KUPATA POINTI MOJA ANFIELD
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Kwa zaidi ya wiki sasa presha ya mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Liverpool  dhidi ya  Man Uni...
Man United vs Liverpool
Kwa zaidi ya wiki sasa presha ya mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Liverpool dhidi ya Man United ilikuwa ikitawala kwa mashabiki wa soka duniani kote, usiku wa October 17 katika dimba la Anfield ndio ilikuwa siku ya kumaliza ubishi wa mchezo huo, Liverpool waliwakaribisha Man United kucheza mchezo wao wa 193 katika historia.
Man United vs Liverpool
Mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Man United ulikuwa unawakutanisha makocha ambao rekodi zao kwa mechi 5 zilizopita Jurgen Klopp amemfunga Jose Mourinho mara 3, sare moja na kapoteza mchezo mmoja, kitu ambacho kiliwafanya mashabiki wengi waamini kuwa Klopp anaweza akapata matokeo tena dhidi ya.
Man United vs Liverpool
Katika mchezo huo uliochezwa Anfield na nafasi kubwa kupewa wenyeji Liverpool kutokana na kuwa nyumbani na rekodi ya kocha wao Jurgen Klopp dhidi ya Mourinho kuwa nzuri umemalizika kwa suluhu ya 0-0, kufuatia matokeo hayo Liverpool na Man United wanakuwa wametoka sare ya 45 katika mechi za EPL na sare ya 52 kwa mechi za mashindano yote waliyowahi kukutana.Vikosi: Liverpool (4-3-3): Karius, Clyne, Matip, Lovren, Milner (Moreno 86), Can, Henderson, Coutinho, Mane, Sturridge (Lallana 60), Firmino (Origi 85).
Akiba wasiotumika: Grujic, Klavan, Lucas, Mignolet.

Manchester United (4-2-3-1): De Gea, Valencia, Bailly, Smalling, Blind, Fellaini, Pogba, Rashford (Rooney 77), Ander Herrera, Young (90+2), Ibrahimovic.
Akiba wasiotumika:: Rojo, Mata, Lingard, Carrick, Romero.

Referee: Anthony Taylor (Cheshire)

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top