Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HIZI NDIZO DALILI 10 ZA KUPENDWA NA MAMA MKWE WAKO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Kwa kawaida mama wakwe wanachukuliwa kuwa na ubaridi hatari kama baridi ya Mbeya. Lakini, kuna baa...
Kwa kawaida mama wakwe wanachukuliwa kuwa na ubaridi hatari kama baridi ya Mbeya. Lakini, kuna baadhi yao ni tofauti kabisa. Wapo wenye uvuguvugu wa kimahaba na upendo usiokuwa na kifani kwa wake wa watoto zao. Wakati huo huo kuna wanawake ambao wanadai kuwa hawana uhusiano mzuri na wakwe zao, lakini kwa chini chini wanatamani sana kuwa na uhusiano mzuri na mama mkwe. Kujua kama umo kwenye kitabu cha moyo wa mheshimiwa mama mkwe, basi hizi ndizo ishara na dalili za kukuonesha hilo:
Mama Diamond na Zari Thebosslady
1. Anapokuulizia mara kwa mara: Baada ya shamrashamra za harusi iliyofana vizuri, mama mkwe anatulia huku akiwa mwenye furaha. Anakupigia simu kuuliza hali yako. Anataka kujua lini utamtembelea. Kwa ufupi unakuwa kama mwanaye kwake na moyo wake umejawa mahaba juu yako.

2. Anapokutembelea muda wowote: Sio kawaida kwa mama ambaye umri wake umesonga kufunga safari ndefu kutoka kijijini kwa ajili ya kumtembelea mwanaye pekee. Wamama wengi wazee – isipokuwa wachache – hawapendelei kuwatembelea watoto wao kwa sababu ya wake zao.

3. Anakutumia au anakuletea zawadi: Anapokutembelea haji mikono mitupu. Anakuletea yule jogoo mwenye kilo 7, kiroba cha mahindi, ndizi, kunde na chochote kizuri kutoka kijijini. Usidhani kuwa hayo anayafanya kwa sababu ya mwanaye wa kiume. Bali ni kwa sababu wewe mke wa mwanaye ni mke alimkubali pia.

4. Anakupigania: Mama mkwe anayekupenda atakupigania na kukutetea kuhakikisha kuwa heshima yako haivunjiki. Hata ukiwa na msuguano na mume wako, utaona anakuwa upande wako na kutuliza mambo.

5. Watu wako ndio watu wake: Tangu ulipoolewa na mwanaye, mama huyu amekuwa karibu sana na watu wako. Yuko karibu na mama yako na shangazi zako. Hakosi shughuli za furaha na huzuni za familia yako.
Mama Diamond na Zari Thebosslady
6. Anataka usaidizi wako wa jikoni: Kuna wageni wamekuja nyumbani kwake, atakuuliza aina ya chakula ambacho ungependelea kipikwe. Hata kama kuna wanawake wengine, bado atasisitiza ushiriki katika upishi. Mara nyingi baadhi ya wanawake hulichukulia kwa mtazamo mbaya jambo hili, lakini ukweli ni kwamba hiyo ni kama cheti unachopewa na mama mkwe.

7. Anapokuzungumzia vizuri mbele ya marafiki zake : Wamama wengine wanapolalamika kuhusu wake wa watoto zao ambao wana muonekano mbaya, kucha za bandia, nywele za bandia na wasioweza kupika chakula cha watu 20, mama mkwe wako yeye anakusifia tu.

8. Anajawa na wasiwasi unapokaa kwa wazazi wako muda mwingi kupitia kiasi: Unapowatembelea ndugu zako na ukakaa huko kwa zaidi ya siku moja, mama huyo hukosa amani. Hujawa na wasiwasi kwamba yumkini umeitelekeza familia. Haachi kukupigia simu kuuliza lini utarudi.

9. Anaheshimu ndoa yako na haingilii mambo yenu: Hamuulizi mwanaye au yeyote kuhusu mambo ya ndoa yenu. Anajiweka mbali lakini tatizo likitokea, anakuwa wa kwanza kuja kuwasaidia.

10. Anakuona kuwa ni chaguo sahihi: Mara nyingi mwanaume ndiye anayefanya uamuzi wa kuoa. Lakini, anapomchagua mtu, mama hulazimika kukubali. Mama mkwe anayekupenda huamini kwamba wewe bado ni chaguo sahihi hata kama miaka mingi imepita tangu ulipoolewa. Hizo ni ishara zitakazokuonesha kuwa mama mkwe anakupenda au la!.
******************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top