Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: DC NGUBIAGAI AVALIA NJUGA MIGOGORO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya Kilwa Christopher Ngubiagai Na.Ahmad Mmow, Lindi. KATIKA kuhakikisha anamali...
Christopher Ngubiagai
Mkuu wa wilaya Kilwa Christopher Ngubiagai

Na.Ahmad Mmow, Lindi.
KATIKA kuhakikisha anamaliza migogoro ya wakulima na wafugaji iliyoanza kujitokeza wilayani Kilwa. Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai ameitaka ofisi ya idara ya mifugo ya halmashauri ya wilaya hiyo kumpelekea nakala ya mihtasari ya mikutano mikuu ya vijiji 22 vilivyoingia kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi na vilivyokubali kuwapokea wafugaji.

Ngubiagai alitoa agizo hilo jana, kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Matandu na Kinjumbi alipokuwa anazungumza na wananchi wa vijiji hivyo kwenye mikutano ya hadhara. 

Ngubiagai ambae licha ya kutaka zoezi hilo lifanyike ndani ya siku 14, pia aliagiza apewe nakala za vibali vilivyotolewa na idara hiyo kwa wafugaji. 

Akieleza sababu za kuziomba nyaraka hizo, mkuu huyo wawilaya alisema ili kuwa nasuluhisho la kudumu la migogoro ya wakulima na wafugaji nimuhimu kujua idadi ya mifugo na wafugaji waliohamia katika vijiji hivyo inalingana na ilivyokubaliwa na wananchi wa vijiji hivyo vilivyoridhia kuwapokea.

Alisema zipodalili kuwa baadhi ya vijiji vimepokea mifugo na wafugaji wengi tofauti na ilivyokubaliwa.
"Naomba pia na vibali mlivyotoa kuwapa wafugaji, ili nijiridhishe kama wafugaji hao wanazingatia masharti ya vibali hivyo," alisisitiza Ngubiagai.

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka watendaji wa vijiji wakukumbushe wakulima waliovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ufugaji waondoke ndani ya wiki walivyotakiwa na halmashauri ya wilaya hiyo.

Huku akiwataka wafugaji kuacha kupeleka na kulisha mifugo yao kwenye maeneo na vijiji visivyotenga maeneo kwa ajili ya mifugo. 

Alisema chanzo cha migogoro ni wakulima na wafugaji kutoheshimu mipaka na matumizi ya maeneo yaliyotengwa. Hivyo yeye asingependa wakulima na wafugaji waishi kwa uhasama na kuvuruga amani iliyopo wilayani humo.

Aliwataka wataalamu wa idara za mifugo na kilimo watoe elimu kwa wananchi kuhusu taratibu,kanuni na sheria za kuwapokea wafugaji katika vijiji vyao.
"Wengi wanawapokea wakiwa hawajui haki zao na za wafugaji ndio sababu wanataka wafugaji wawaondolewe kwenye vijiji ambavyo wamesajiliwa nakuwa wakazi halali kama wao, jambo ambalo haliwezekani. Maana nikinyume cha sheria," alisema.

Pia Ngubiagai ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo, alitoa wito kwa wanasiasa waache tabia ya kuwahaidi wananchi mambo yasiyowezekana kutekelezeka kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria za nchi kwa lengo la kuwafurahisha ili wapigiwe kura wakati wanaomba nafasi mbalimbali za uongozi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top