Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: ALICHOKISEMA ZITTO KABWE KUHUSU WALIOTUMBULIWA MAJIPU NA RAIS MAGUFULI HICHI HAPA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
KIONGOZI wa chama cha ACT–Wazalendo, Zitto Kabwe , amemshauri Rais John Magufuli , kuwafikisha kwe...
KIONGOZI wa chama cha ACT–Wazalendo, Zitto Kabwe, amemshauri Rais John Magufuli, kuwafikisha kwenye vyombo vya nidhamu na sheria wote aliowatumbua tangu alipoingia madarakani.
Zitto Kabwe
Alisema watu hao waliotumbuliwa kuanzia mwaka jana hadi Agosti mwaka huu, ambao idadi yao ni takribani 130, wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria na nidhamu ili viwaeleze Watanzania kuhusu kile wanachotuhumiwa nacho watumishi hao.


Halikadhalika alimshauri Rais Magufuli kufuata misingi ya haki na usawa katika kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wa umma aliowatumbua kwa tuhuma mbalimbali.

Zitto aliyasema hayo jana Dar es Salaam katika mkutano mkuu wa ACT-Wazalendo, unaojadili mambo kadhaa yakiwamo, hali ya siasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 pamoja na uzoefu wa kisiasa wa mataifa mengine ya Afrika.

****************
COLLABO YA VANNESA MDEE NA TREY SONGZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top