Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: ZUNGU AMUOMBA RADHI MBOWE BUNGENI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amemuomba radhi kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Fre...
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amemuomba radhi kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kwa kushindwa kutambua mchango wake kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mussa Zungu
Hatua hiyo imefuatia mwongozo ulioombwa na wabunge wawili Chadema, kuwa mchango wa Mbowe haukutambulika licha ya kufika Bukoba, kutoa misaada na kushirikiana na waathirika wa tukio hilo hadi sasa.

Aliyeanza kuomba mwongozo ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche ambaye alihoji kwa nini mwenyekiti huyo wa Bunge amewatambua viongozi waliofika eneo la tukio na kutoa misaada lakini ameshindwa kumtambua Mbowe ambaye mpaka sasa yupo eneo la tukio na ametoa msaada.

Mbunge mwingine ni Pascal Haonga wa Mbozi ambaye alisema Mbowe ni kiongozi mkubwa na halitakuwa jambo la maana kama mchango wake hautatambulika kwani suala hilo siyo la kisiasa.

Kufuatia mwongozo huo, Zungu aliomba radhi na kuongeza kuwa anamtambua Mbowe kama kiongozi aliyetoa msaada kwa waathirika hao.
__________________________________________
ENJOY NA HII REMIX YA “ALL THE WAY UP” AMBAYO IMEFANYWA NA DIAMOND PLATNUMZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top