Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI SALA YA PAMOJA KUWAAGA MAREHEMU WA TETEMEKO LA ARDHI MJINI BUKOBA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiwasili katika uwanja wa mpira wa Miguu wa Kaitaba mjini Bukoba...
tetemeko la Ardhi
Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiwasili katika uwanja wa mpira wa Miguu wa Kaitaba mjini Bukoba mapema leo,kwa ajili ya kuwapa pole nyingi wakazi wa mji huo na kwingineko na pia kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokuwa wamekumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.

Tetemeko hilo kubwa la ardhi lenye mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea jana Septemba 10, 2016 katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kadhalika nchi za Burundi na Uganda.Mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyopata athari kwa mujibu wa taarifa ni Mwanza, Mara na Kagera nchini na kuripotiwa kuua zaidi ya watu 15 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa sambamba na kubomoa majengo mbalimbali.
tetemeko la Ardhi
Pichani kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu ,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.
tetemeko la Ardhi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mbunge wa jimbo la BUkoba Mjini,Mh Wilfred Lwakatare,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.
tetemeko la Ardhi
Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga wapendwa wao.
tetemeko la Ardhi
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa dini wakiwa katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuaga miili ya marehemu waliokumbwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.
tetemeko la Ardhi
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya marehemu walioathiriwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top