Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: VITA VYA SINGEL:: SHOLO MWAMBA AMPA MAKAVU MAN FONGO NA KUSEMA ANATAFUTA KIKI, NI ISHU YA MAMA WEMA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Sahau kuhusu Bongo Fleva – sasa ulingo umevamiwa na wasanii wa Singeli. Mfalme wa muziki wa Singeli...
Sahau kuhusu Bongo Fleva – sasa ulingo umevamiwa na wasanii wa Singeli. Mfalme wa muziki wa Singeli, Sholo Mwamba amefunguka baada ya mfalme mwenzie, Man Fongo kumtuhumu msanii huyo kuwa ndiye aliyesababisha kutoelewana kati yake na Wema Sepetu baada ya kufikisha taarifa za umbea.
Sholo Mwamba
Muimbaji huyo amesema kuwa Man Fongo anatafuta kiki kwakuwa amezoea kuropoka.
“Mdogo wangu anatafuta kiki, huu ni muziki anatakiwa afanye kazi mambo mengine yaendelee. Yule alikuwa Dj wangu [Man Fongo] kwahiyo sina matatizo naye.”

“Sitaki kumtafuta kwa sababu anaweza kuzusha kuwa nimempigia simu nimemuomba collabo,” ameongeza.
Man Fongo
Msanii huyo amedai kuwa yeye hakumpigia simu mama Wema wala hiyo namba yake ya simu hajawahi kuwa nayo na amewahi kuonana naye mara moja tu.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top