Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: U-HEARD! BAADA YA VIDEO YA “RARUA” KUTOKA,HILI NDILO POVU LA EDDY (EX BOYFRIEND WA MALAIKA)
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Wiki kadhaa zilizopita tulizisikia stori za magomvi ya mwanadada Malaika na aliyekuwa mpenzi wake...
Wiki kadhaa zilizopita tulizisikia stori za magomvi ya mwanadada Malaika na aliyekuwa mpenzi wake Eddy.

Malaika
Magomvi hayo yalifika mpaka katika vyombo vya dola na kuzua kesi nzito ambayo hadi silaha za moto zilihusika ndani yake.

Eddy alikuwa pia ni msimamizi wa mwanadada Malaika katika shughuli zake za kimuziki kiasi kwamba hata mtonyo wa video ya “Rarua” Eddy amehusika.

Katika magomvi hayo tulizinyaka za Eddy kuizuia video ya “Rarua” kutoka, na huenda ndio ikawa sababu kuu ya kuisababisa video hiyo kuchelewa. 


Wiki iliyopita Mwanadada Malaika aliiachia rasmi video hiyo.

Bila kupoteza muda Soudy Brown akaamua amvutie waya Eddy ilikujua kuhusiana na suala hilo. Labda matatizo ya wawili hao yamekwisha au kuna kingine nyuma ya pazia.

Eddy alichomjibu Soudy Brown ni kwamba “Hanscana anawashwa”. Hilo ni moja kati ya mapovu ambayo Eddy amefunguka kuhusu kitendo hicho cha Malaika kuiachia video ya “Rarua”. Lawama zote amemtupia Director Hanscana.

Sitaki kukunyima uhondo ili ujute kunifahamu, ubuyu wote nimekuwekea katika hii video hapa chini na sioni kama una sababu ya kukosa kuitazama video hii.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top