Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: TANZIA: AFISA HABARI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI NDG CLARENCE CHILUMBA AFARIKI DUNIA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
AFISA HABARI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI NDG CLARENCE CHILUMBA ENZI ZA UHAI WAKE. MKURUG...
clarence Chilumba
AFISA HABARI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI NDG CLARENCE CHILUMBA ENZI ZA UHAI WAKE.

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI BI.GIMBANA EMANUEL NTAVYO, ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA AFISA HABARI NDG. CLARENCE CHILUMBA KILICHOTOKEA LEO TAREHE 02/09/2016, NDG. CHILUMBA ALIPATA AJALI YA PIKIPIKI SIKU YA TAREHE 31/8/2016 MAJIRA YA JIONI MJINI MASASI WAKATI AKITOKEA KAZINI KUELEKEA NYUMBANI KWAKE.BAADA YA KUPATA AJALI ALIWAHISHWA HOSPITALINI MKOMAINDO AMBAPO ALIPATA HUDUMA YA KWANZA NA BAADAYE KUPELEKWA NDANDA. AKIWA NDANDA HALI YAKE ILIZIDI KUWA MBAYA, TAREHE 1/9/2016 ALIPATA RUFAA YA KWENDA MUHIMBILI, AMEFARIKI AKIWA NJIANI SOMANGA O2/9/2016 MAJIRA YA SAA 8:25 USIKU

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI

AMINA.

TAARIFA ZA MAZISHI ZOTATOLEWA BAADA YA KUWASILIANA NA NDUGU WA MAREHEMU.

IMETOLEWA NA.
OFISI YA MKURUGENZI WA MJI
MASASI

Septemba,02,2016.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top