Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: TAARIFA ZA KIFO CHA MUHOGO MCHUNGU NI ZA UZUSHI, MWENYEWE AFUNGUKA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Abdallah Makumbila alimaarufu kama Muhogo Mchungu...
Muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Abdallah Makumbila alimaarufu kama Muhogo Mchungu amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki na kusema kuwa yeye saizi hasumbuliwi hata na mafua.
Muhogo Mchungu
Muhogo Mchungu alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Supamix cha East Africa Radio amesema kuwa kwa sasa anafanya utaratibu wa kwenda kumshtaki mtu ambaye amesambaza taarifa kwenye mitandao kuwa yeye amefariki dunia.
"Mimi ni mzima wa afya njema kabisa mimi si marehemu kama watu wanavyosema ndiyo maana saizi Zembwela unaongea na mimi, saizi nipo Bagamoyo mzima wa afya njema kabisaa na katika wiki mbili hizi sijasumbuliwa hata na mafua, hata mimi nimesikia hizo taarifa za kifo changu na nimetumiwa mpaka picha, sasa sijui huyo alizusha hayo mambo alikuwa na maana gani, maana amezua taharuki kwenye familia yangu na katika jamii hivyo saizi nataka kwenda TCRA ili tuweze kumjua nani amefanya hivyo ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria" alisema Muhogo Mchungu.
Mbali na hilo Muhogo Mchungu amesema kuwa mitandao ya kijamii ni kama kisu ukiitumia vibaya inaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii na kuwataka watu wataumie vyema mitandao ya kijamii ili wasilete madhara kwa jamii.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top