Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: SAUTI SOL WAIZIMIKIA SALOME YA DIAMOND PLATNUMZ NA HICHI NDICHO WALICHOKISEMA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Muziki ni hisia na kila mmoja anaamua kufanya kile anchojisikia bila kujali wengine watatafsiri vip...
Muziki ni hisia na kila mmoja anaamua kufanya kile anchojisikia bila kujali wengine watatafsiri vipi, Hiyo ni sawa na alichokifanya Bongoflava icon Diamond Platnumz kwenye hitsong Salome ambayo amemshirikisa mtu mbaya Rayvanny kutoka WCB.
Diamond Platnumz ft Rayvanny - Salome
Ndani ya siku mbili tayari Salome imekua ni ngoma kubwa ambayo inaongelewa kila kona kwa uzuri na ubaya.

Kundi la muziki “Sautisol” la nchini Kenya limetumia ukurasa wake wa Instagram kuyaelezea mahaba yao kwenye ngoma hiyo baada ya kutundika picha ambayo ni moja kati ya Scenes zilizoonekana kwenye Video hiyo y  “Salome” ikiwa na maelezo yaliyosomeka:

Katika tafsiri ya Kiswahili : "Ni Bora Dunia ingejua kiswahili, maana hii ngoma ni matatizo… #salome @diamondplatnumz x @rayvanny #TraditionalVersion."

Huenda salome ikawa moja kati ya ngoma za kiswahili zenye ushawishi mkubwa siku za mbele na tusishangae kuona au kusikia imefanywa covers nyingi kulio ngoma yeyote ya Bongoflava.

_______________________________________
TAZAMA HAPA SHOW YA USIKU WA VIGOMA JIJINI TANGA, WEMA SEPETU AKIKATA MAUNO.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top