Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: SAIDA KAROLI KUJAZWA MAPESA NA WIMBO WA SALOME WA DIAMOND PLATNUMZ, MWENYEWE AFUNGUKA HAYA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Diamond amedai kuwa Saida Karoli atapata asilimia 25 ya mapato ya wimbo wa Salome . Diamond ame...
Diamond amedai kuwa Saida Karoli atapata asilimia 25 ya mapato ya wimbo wa Salome.
Diamond na Rayvanny
Diamond amerudia baadhi ya vitu kwenye wimbo wake mpya ‘Salome’ aliomshirikisha Raymond kutoka kwenye wimbo wa ‘Maria Salome’ wa Saida Karoli uliotoka takribani miaka 16 iliyopita.

Akiongea na 255 ya Clouds FM Jumatatu hii, hitmaker huyo wa Kidogo amesema kuwa walizungumza na uongozi wa Saida Karoli na kumpatia kiasi cha fedha pamoja na asilimia 25 ya publishing ya wimbo huo.

“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata percent,” amesema Diamond.

Mpaka sasa video ya ‘Salome’ ya Diamond ina siku mbili tangu ilipoachiwa kwenye mtandao wa YouTube lakini imefanikiwa kutazamwa mara 698k (
698,558).

__________________________________________
ENJOY NA HII REMIX YA “ALL THE WAY UP” AMBAYO IMEFANYWA NA DIAMOND PLATNUMZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top