Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MTENDAJI MKUU WA TTCL NA KUMTEUA HUYU HAPA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Kufuatia hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia mwenza wa K...
Rais Magufuli

post
Kufuatia hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na hivyo Serikali kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Waziri Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.

Bw. Waziri Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo tarehe 23 Septemba, 2016.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

23 Septemba, 2016

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top