Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: RAIS BONGO AKUBALI KURA ZIHESABIWE UPYA GABON
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Gabon, Ali Bongo , amesema yuko tayari kutii uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba iwapo mahakama...
Rais wa Gabon, Ali Bongo, amesema yuko tayari kutii uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba iwapo mahakama hiyo itaagiza kura za uchaguzi mkuu uliofanyika wiki mbili zilizopita zihesabiwe upya.
Ali Bongo
Waangalizi wa kimataifa wamesema kuna kasoro nyingi kwenye matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa, ambayo yalimpa Bw Bongo ushindi mwembamba.

Kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Ufaransa, Bw Bongo amesema sheria za nchi zake haziruhusu kura zihesabiwe tena.

Hata hivyo, alisema atakubali hilo iwapo mahakama itaamua hilo lifanyike.

Mahakama ya kikatiba inatarajiwa kukutana Alhamisi kuangazia kesi ya kupinga matoke ya uchaguzi huo ambayo iliwasilishwa na mgombea wa upinzani, Jean Ping.

Bw Bongo alisema suala kuu kwake kwa sasa ni kurejesha utulivu nchini humo na kuiwezesha Mahakama ya Kikatiba ifanye kazi yake.

Ali Bongo alitangazwa mshindi wa uchaguzi, lakini upinzani ukiongozwa na Jean Ping ulipinga matokeo.

Bw Bongo alipata 49.8% ya kura naye Bw Ping akiwa na 48.2%, tofauti kati yao ikiwa kura 5,594.

Bw Ping alishinda majimbo sita kati ya tisa na ameomba kurudiwa tena kwa shughuli ya hesabu ya kura.

Katika jimbo la Haut-Ogooue, anakotoka Bw Bongo, waliojitokeza kupiga kura walikuwa 99.93% kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na 95% ya kura zilipigwa kwa rais huyo.__________________________________________
ENJOY NA HII REMIX YA “ALL THE WAY UP” AMBAYO IMEFANYWA NA DIAMOND PLATNUMZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top