Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: OFISI YA MAKAMU WA RAIS YATOLEA TAARIFA, TAARIFA YA KUJIUZULU KWA MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu. YAH: KUKANUSHA TAARI...
Samia Suluhu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu.

Post

YAH: KUKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII

Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.

Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki. Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.


Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais


_____________________________________________________________________________
ENJOY NA HII REMIX YA “ALL THE WAY UP” AMBAYO IMEFANYWA NA DIAMOND PLATNUMZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top