Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: NI ENRIQUE NA SIMEONE AU MESSI NA GRIEZMANN LEO NDANI YA LA LIGA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya mechi za wiki ya nne La Liga kuendelea wikiendi iliyopita, leo ligi hiyo itaendelea kwa m...
Baada ya mechi za wiki ya nne La Liga kuendelea wikiendi iliyopita, leo ligi hiyo itaendelea kwa mechi takribani tano kuchezwa ambapo mechi zitakazo vuta hisia za wengi ni kati ya Real Madrid dhidi ya Villareal na Barcelona dhidi ya Atletico Madrid.
Barcelona Vs Atletico Madrid.
BARCA Vs ATLETICO
Moja ya mechi kubwa za msimu kwenye La Liga ambapo hesabu kuu za mchezo huu zitakuwa chini ya waalimu Luis Enrique na Diego Simeone ambao wanatakiwa kujua namna ya kuzichanga karata zao kwasababu wote wana vikosi imara.
Barcelona
Baada ya kupoteza dhidi ya Alaves, Enrique hakutaka tena kuwaacha nje nyota wake kama Iniesta, Messi na Suarez ambao wote walianza kwenye mechi dhidi ya Celtic na Leganes na kupata ushindi mnono. 

Hivyo kwa upande wa Barcelona hakutakuwa na mabadiliko sana.
Atletico Madrid
Atletico Madrid haikuanza vyema msimu huu lakini katika mechi mbili za mwisho imerejea vyema na inaonekana muunganiko wa wachezaji kama Griezmann, Saul, Gameiro na Carrasco unaendelea kuimarika na huenda Simeone anaweza asipate taabu ya kupanga kikosi na akatumia nyota wawili katika safu ya ushambuliaji ambao ni Griezmann na Gameiro.


RATIBA MECHI ZA LEO JUMATANO
Celta Vigo vs Gijon saa saa 3:00 Usiku

Real Madrid Vs Villareal saa 3:00 Usiku
Granada Vs Bilbao saa 5:00 Usiku
Real Sociedad Vs Las Palmas Saa 5:00 Usiku
Barcelona Vs Atletico Madrid Saa 5:00 Usiku
_______________________________________
TAZAMA HAPA SHOW YA USIKU WA VIGOMA JIJINI TANGA, WEMA SEPETU AKIKATA MAUNO.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top