Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MKUU WA WILAYA ATOA AGIZO LA KUKAMATWA KWA MRATIBU WA ELIMU NA ASIKARI MGAMBO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Kilwa Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai ameliagiza jeshi la Polisi wila...
Na. Ahmad Mmow, Kilwa
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai ameliagiza jeshi la Polisi wilayani humo liwakamate Mratibu Elimu wa kata ya Namayuni na Asikari Mgambo wa kijiji cha ngorongoro.

Ngubiagai
Ngubiagai alitoa agizo hilo baada ya kusikia malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Nahamawaliemueleza kwamba mratibu kata huyo, Claudis Sanzala alishirikiana na asikari mgambo, Alfonce Kipengele kumtorosha kijana anaetuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Namayuni.

Ngubiagai alisema kitendo cha kutoroka kwa mtuhumiwa huyo mikononi mwa mratibu na asikari huyo ambao walikabidhiwa na Mtendaji wa kata hiyo wampeleke katika kituo kidogo cha polisi cha Somanga hakikubaliki.

Alisema tatizo la wanafunzi kupewa mimba katika wilaya hiyo ni kubwa hivyo atawachukulia hatua za kisheria wanaoshiriki vitendo hivyo na wanaowalinda.
"Hao wakamatwe ili wahojiwe tujue walitorokwaje, kama majibu yao hayataeleweka itabidi wafikishwe mahakamani. Nakuagiza OCD hao watu nataka niwakute rumande, hatuwezi kuwalea watu wachache wanaokwamisha juhudi za serikali. watuambie aliwatorokaje, alikuwa mikononi mwao lazima wawajibike kwa hilo". alisisitiza Ngubiagai.

Pamoja na agizo hilo Ngubiagai ametoa wiki mbili kwa ofisi ya kata hiyo kuaandaa na kumpa taarifa ya matumizi ya shilingi 15.00milioni zilizotolewa na halmashauri ya wilaya hiyo ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za wananchi wa kijiji cha Nahamawalioamua kujenga zahanati ya kijiji chao.

Awali wananchi hao walimweleza mkuu huyo wa wilaya wahalifu wengi wanaofikishwa kwenye ofisi ya kata ya Namayuni wamekuwa wakitoroka katika mazingira ya kutatanisha kabla ya kufikishwa katika kituo kidogo cha polisi cha Somanga. 

Vile vile wananchi hao walimueleza kutoridhishwa na matumizi ya fedha za shughuli za maendeleo vijijini zinazopitia kwenye ofisi ya kata ya namayuni.
"Hapa zimeletwa shilingi Milioni kumi na tano, ofisi ya kata inasema taarifa ya matumizi yake tutapewa na mtendaji wa kijiji, na yeye anasema hajui na hajapewa taarifa ya matumizi ya fedha hizo na Ofisa Mtendaji Kata wake, hali hiyo siyo mara moja kufanyika kwa fedha za maendeleo zinazopitishwa katika ofisi ya kata," alisema mmoja wa kazi wa kijiji hicho cha Nahama, Saidi Abdallah.

Ngubiagai yupo katika ziara ya kikazi katika vijiji vya wilaya hii ili kuhimiza shughuli za maendeleo. ambapo ameshatembelea vijiji 6 kati 90 vinavyo unda wilaya ya Kilwa.
__________________________________________
ENJOY NA HII REMIX YA “ALL THE WAY UP” AMBAYO IMEFANYWA NA DIAMOND PLATNUMZ

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top