Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MENEJA CRDB, RAS PAMOJA NA MAKONDA WAFIKISHWA MAHAKAMANI
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Aliyekuwa Ofisa tawala Mkoa wa Kagera (RAS) Bw Amantius Msole , Aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa...
kagera tetemeko
Aliyekuwa Ofisa tawala Mkoa wa Kagera (RAS) Bw Amantius Msole, Aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba BW Kelvin Makonda, Aliyekuwa Mhasibu wa Mkoa Kagera Simbaufoo Swai na Meneja CRDB Kagera Karlo Sendwa wamefikishwa mahakamani Jana mchana kwa kutengeneza account bandia iliyo na jina sawa na ilioandaliwa na serikali kukusanya fedha kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko mkoani Kagera.

Wakati ya serikali ikiitwa KAMATI MAAFA KAGERA ikiwa na kianzio cha 0152..wao wamefungua ya jina hilo hilo lakini ikiwa na kianzio cha 0150...Kwa hiyo ya Serikali iliyopitishwa ni 0152225617300 CRDB Bukoba Huku bandia ina jina hilo hilo lakini ikiwa na tofauti ya namba moja tu yahani 0150225617300.
kagera tetemeko
Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote na wamenyimwa dhamana hadi septemba 30, 2016 itakapotajwa tena.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top