Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MANCHESTER UNITED NA MANCHESTER CITY KUKUTANA TENA RAUNDI YA NNE EFL CUP, BAADA YA KUSHINDA LEO
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Manchester United wakiwa Ugenini huko Sixfields Stadium Jijini Northampton kwenye Mechi ya Raundi...
Manchester United wakiwa Ugenini huko Sixfields Stadium Jijini Northampton kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya EFL CUP, Kombe la Ligi, wameitwanga Timu ya Daraja la Ligi 1 Northampton Town Bao 3-1 na kutinga Raundi ya 4.
Manchester United
Man United walitamgulia kufunga kwa Bao la Michael Carrick na Northampton kusawazisha kwa Penati iliyopigwa na Revell.

Hadi Mapumziko Northampton 1 Man United 1.


Kipindi cha Pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko lakini Manchester United yalikuwa na faida kwao kwani waliweza kupata Bao mbili na kufanya Matokeo kuwa 3-1 mabao ambayo yalifungwa na Herrera na Rashford.
Man City
Nao Mabingwa Watetezi wa Kombe hili la Ligi, Man City, pia wameingia Raundi ya 4 kwa kuifunga Swansea City Bao 2-1 kwa Bao za Gael Clichy na Garcia Serrano na Swansea kufunga kupitia Gylfi Sigurdsson.
Manchester Manager
Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 4 imefanyika Usiku huu na Hii ndio Ratiba kamili.
West Ham vs Chelsea
Man United vs Man City
Arsenal vs Reading
Liverpool vs Tottenham
Bristol City vs Hull
Leeds vs Norwich

Newcastle vs Preston
Southampton vs Sunderland
Kwa Ratiba hiyo inamaanisha kutakuwepo na Derby nyingine ya Manchester ambayo itachezwa kwenye uwanja wa Oldtraford baada ya ile ya Ligi Kuu ambayo manchester City waliibuka washindi kwa goli 1-0.

VIKOSI VILIVYOANZA:
Northampton: Smith; Moloney, Buchanan, Diamond, Zakuani; Gorre, McCourt, Hoskins, Beautyman, Taylor; Revell
Akiba: Cornell, Byrom, Richards, Potter, Sonupe. O’Toole, Nyatanga

Man United: Romero; Fosu-Mensah, Smalling, Blind, Rojo; Schneiderlin, Carrick, Herrera; Memphis, Rooney, Young
Akiba: Johnstone, Darmian, Fellaini, Lingaard, Mata, Rashford, Ibrahimovic

REFA: Stuart AttwellMATOKEO YA EFL CUP RAUNDI YA 3: JUMANNE SEPTEMBA 21
Swansea City 1 - 2 Man. City
Northampton 1 - 3 Man United
Southampton 2 - 0 Crystal Palace
QPR 1 - 1 Sunderland
West Ham 1 - 0 Stanley
Fulham 1 - 2 Bristol City
Stoke City 1 - 2 Hull City
Tottenham 5 - 0 Gillingham

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top