Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: MAN UNITED YAWATWANGA MABINGWA LEICESTER, POGBA AFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI!
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
MANCHESTER UNITED Leo wakiwa kwao Old Trafford wamewatandika Mabingwa wa England Leicester City...
Man United
MANCHESTER UNITED Leo wakiwa kwao Old Trafford wamewatandika Mabingwa wa England Leicester City kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ambayo Kepteni wao Wayne Rooney alianzia Benchi.
Man United
Man United waliandika Bao la Kwanza Dakika ya 22 kupitia Chris Smalling na kisha ndani ya Dakika 5, katika Dakika za 37, 40 na 42, Juan Mata, Marcus Rashford na Paul Pogba walipiga Bao huku Pogba akifungua akauti yake ya Magoli kwenye EPL.
Man United
Hadi Mapumziko, Man United 4 - 0 Leicester.
Leicester
Kipindi cha Pili, Leicester waliwatoa Masta wao Jamie Vardy na Riyad Mahrez na kuwaingiza Demaray Gray na Andy King na kupata Bao lao pekee kupitia Gray katika Dakika ya 59.
Claudio Ranieri and Jose Mourinho
VIKOSI:Manchester United (Mfumo 4-2-3-1): De Gea; Valencia, Bailly, Smalling, Blind; Herrera, Pogba; Lingard [Carrick, 78’], Mata [Young, 87’], Rashford [Rooney, 83’], Ibrahimovic.
Substitutes: Romero, Rojo, Fosu-Mensah, Carrick, Fellaini, Young, Rooney.

Leicester City (Mfumo 4-4-2): Zieler; Simpson, Morgan, Huth, Fuchs; Mahrez [Andy King, 46’], Drinkwater, Amartey, Albrighton [Schlupp, 62’]; Slimani, Vardy [Demaray Gray, 46’].
Substitutes: Hernández, King, Hamer, Schlupp, Okazaki, Gray, Ulloa.

REFA: Mike Dean

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top