Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: KUNA WAIGIZAJI WENGI WAZURI HAWAPEWI NAFASI - JB
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa filamu nchini Jacob Steven (JB) amefunguka na kusema kuwa kuna wasanii wengi wachanga n...
Msanii wa filamu nchini Jacob Steven (JB) amefunguka na kusema kuwa kuna wasanii wengi wachanga ni wazuri katika tasnia ya filamu nchini lakini hawapewi nafasi ya kuonesha uwezo wao wa kuigiza ndiyo maana tasnia hiyo imekuwa na wasanii walewale.
Jacob Steven (JB)
Akiongea kwenye kipindi cha 5Selekt, Jacob Steven (JB) alisema kwa sasa kupitia kampuni yake ya Jerusalem atafanya mpango wa kuhakikisha anazalisha vipaji vingi vipya ambavyo vitaleta changamoto kwenye tasnia ya filamu nchini.
"Ni kweli nataka kustaafu kuigiza ila nitakuwa nyuma ya camera kama mwongozaji, nitahakikisha nazalisha vipaji vingi kwani kwenye filamu huku kuna wasanii wengi wachanga wanaweza sana na wana vipaji lakini hawapati nafasi ya kuonesha uwezo wao. Hata huku kwenye filamu wapo wasanii wengi ni maarufu sana lakini hawana uwezo mkubwa wa kuigiza kama wasanii wachanga" alisema Jacob Steven

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top