Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA YALAUMIWA KUVIKOSESHA USHURU AMCOS
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
NA. Ahmad Mmow, Nachingwea Nia njema ya Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi ya Kuvita...
NA. Ahmad Mmow, Nachingwea
Nia njema ya Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi ya Kuvitaka vijiji na kata za wilaya hiyo vipate ushuru sitahiki wa mazao mchanganyiko umetajwa kuvikosesha ushuru vyama vya msingi vilivyopo wilayani humo.
Nachingwea
Hayo yalielezwa jana  na mwenyekiti wa kamati ya chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, Abdulaziz Liega kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha walimu Nachingwea.

Liega alisema kitendo cha halmashauri hiyo kuwapa haki watendaji wa kata ya kutoa hati za kusafirishia mazao (PDN) wafanyabiashara kimesababisha vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) kukosa mapato yanayotokana na ushuru, alisema uamuzi huo umesababisha wafanyabiashara kukwepa kwenda kulipa kwenye vyama vya ushirika na kupewa hati za kusafirishia za vyama hivyo.

Liega ambae chama chake kipo kwenye mchakato wa kusajiliwa, alisema ingawa vyama vya msingi vinahati za kusafirishia lakini wafanyabiashara na watendaji wa kata wanakiuka makubaliano yanayowataka wasipewe hati za kusafirishia mazao(PDN) na watendaji kata kabla ya kupewa hati za vyama vya msingi vya ushirika.
"Sasa hivi vyama vya msingi vipo hoi havipati ushuru, ukiwauliza wafanyabiashara wanasema tuwasiliane na halmashauri ya wilaya, jambo ambalo nikinyume na dhamira ya mfumo huo," alisema Liega.

Mwenyekiti huyo alisema vyama vya msingi vipo kwa mujibu wa sheria na vinalipa kodi. Hivyo vinastahili kupata ushuru na havitakiwi kuingiliwa kwa madai kuwa vyama vinataratibu, kanuni na sheriazake.
"Kama lengo nikudhibiti mapato basi sasa halmashauri inaibiwa na vyama vya ushirika vinakosa ushuru, kwa sababu uzito wa mazao unaolipiwa nitofauti nayanayosafirishwa," alisema Liega.

Akijibu malalamiko hayo, mwenyekiti wa halmashauri wilaya ya Nachingwea, Ahmad Makoroganya, alisema lengo la kuwapa uwezo watendaji wa kata ni kudhibiti mapato na kutaka vijiji na kata zipate ushuru unaositahili.

Alisema watendaji kata walishaambiwa wasitoe hati hizo kwa wafanyabiashara bila kuziona hati walizopewa na vyama vya msingi.
"Kama hali ipo hivyo nitafuatilia, kwa sababu hayo sio waliyoelezwa hao watendaji," alisema Makoroganya

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top