Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: DC NGUBIAGAI AISHUKIA IDARA YA ARDHI HALMASHAURI YA KILWA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai. Na.Ahmed Abdallah, Kilwa. Mkuu ...
Christopher Ngubiagai
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai.

Na.Ahmed Abdallah, Kilwa.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, Christopher Ngubiagai aimepa siku 30, idara ya ardhi ya halmashauri ya wilaya hiyo imalize mgogoro wa mpaka baina ya vijiji vya Mandawa na Milumba.

Ngubiagai alitoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara wakati alipozungumza na wananchi katika kijiji cha Mandawa, uliofanyika jana kijijini hapo.

Baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na viongozi wa kijiji hicho na kata ya Mandawa, ambao waliituhumu idara hiyo kuwa inachochea mgogoro huo.

Alisema baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi hao alibaini kuwa halmashauri kupitia idara hiyo haikuwajibika ipisavyo kumaliza mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka nane. Badala yake kulikuwa na uzembe.

Hivyo aliitaka idara hiyo kumaliza mgogoro huo ndani ya siku 30 kuanzia siku anatoa agizo hilo.

Ngubiagai ambae yupo ziara ya kikazi katika vijiji vya wilaya hiyo ili kuhimiza kazi za maendeleo, alisema baadhi ya watumishi wa umma ni chanzo cha migogoro katika jamii ili wajinufaishe nayo badala ya kutimiza wajibu wao wakutatua.

Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kwamba hatawaonea aibu watumishi wazembe na wala rushwa katika wilaya hiyo.

Huku akiwasihi watumishi wenye tabia hiyo wawahurumie wananchi wanyonge wanaowatumikia. Naiwapo hawana huruma basi walau watakeleze masharti ya mikataba ya ajira zao yanayowataka wafanye kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma.

"Sisi tunalipwa mishahara kutokana na kodi zinazolipwa na wananchi hawa, lakini hatutaki kutimiza wajibu wetu kwao. Sitamuogopa mtumishi yeyote katika wilaya hii ambae anawaumiza wananchi na asietimiza wajibu wake," alisema Ngubiagai.

Pia mkuu huyo wa wilaya viongozi wa serikali za vijiji kuunda madawati ya kusikiliza kero na malilamiko ya wananchi, sanjari na kutenga siku maalumu za kusikiliza kero na malalamiko.

Ambapo yeye ametenga siku ya alhamusi ya kila wiki kuwa ni siku ya kusikiliza malalamuko na kero katika ofisi yake.

Awali wananchi na viongozi wa kijiji hicho wakiongozwa na diwani wa kata ya Mandawa, Swahaba Matajiri(CUF), walimueleza mkuu huyo wa wilaya kwamba idara nyingi za halmashauri ya wilaya hiyo haziwajibiki ipasavyo katika kushugulikia matatizo na mahitaji ya wananchi.

Hivyo walimtahadharisha akitaka wilaya hiyo iweze kuwa na maendeleo na afanye kazi kwa furaha katika kipindi cha uongozi wake, hana budi kuanza kuisafisha halmashauri hiyo. 

Kwa upande wake ofisa wa idara ya ardhi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Abinel Mathias licha ya kukiri kuwepo mgogoro huo, alisema wananchi wenyewe wa vijiji hivyo ndio chanzo cha mgogoro.

Kwamadai kuwa hawataki kufuata na kukubali mipaka iliyopo kwenye ramani ambayo pande zote ziliridhia itumike katika kubainisha mipaka baina ya vijiji hivyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top