Lindi Yetu Lindi Yetu Author
Title: BAADA YA KUFUNGIWA KITUO CHEDIO "RADIO 5" CHA TOA TAMKO HILI HAPA
Author: Lindi Yetu
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutangaza kuvifungia kwa muda us...
Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya redio, Radio 5 na Magic FM kwa tuhuma za uchochezi, Radio 5 wametoa kauli kwa mashabiki wake juu ya tukio hilo.
Radio 5
Radio 5 kupitia facebook, wametoa taarifa hii.
Good Morning Tanzania.
Habarini Wapendwa wetu kupitia Mitandao yetu ya Kijamii. Baada ya Kimya cha Siku kadhaa Tumerudi Rasmi kuendelea Kukuhabarisha Wewe Mpendwa Msikilizaji / Mfuatiliaji wa Radio 5.
Tunapenda Kuthibitisha kuwa Hatutakua Hewani kwa Kipindi ambacho Bado Hakijulikani, Baada ya Kujiridhisha Ya Kuwa Tumefungiwa “Kurusha Matangazo Hewani” ila bado tunaruhusiwa Kuendelea Kuwahabarisha kupitia Mitandao Yetu ya Kijamii, hivyo Tunapenda Kuchukua Nafasi hii Kuwashukuru Nyie kwa Kuendelea Kuwa Nasi katika Kipindi Hiki Kigumu na Kifupi.
Endelea Kupata Taarifa na Matukio yote (Habari, Burudani, Michezo n.k) Yanayojiri Hapa Nchini na Nje ya Nchi Kupitia Kurasa Zetu za Facebook, Twitter na Instagram ambapo Kote Tunapatikana kupitia @Radio5tz .
Kaa Mkao wa Kula Kuna Mengi Mazuri Yanakuja Kupitia Kurasa Hizi. Ahsanteni Sana kwa Suppoti Yenu na Endeleeni Kuwa Nasi.Tunashukuru.#Radio5tz

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

 
Top